MPENZI KIKOJOZI

MPENZI KIKOJOZI (1)
0742873299 WHATSAPP/SMS/CALL
Emmy alikuwa na kila uzuri ,mwonekano wake ulikuwa ukivutia kupita maelezo ,wengi walipenda kumwita malaika,ilifika hata kipindi waalimu wake walikuwa wakimweka mbele ya darasa kwani uwepo wake pale ulikuwa ni kivutio tosha ,hata shule ilipopata wageni Emmy ndio alikuwa mhudumu namba moja hakika Emmy alikuwa na sifa zote za uzuri ,Emmy kwa sura alikuwa ni maji ya kunde hakuwa mweupe wala mweusi ,shepu yake ilikuwa imejijenga vyema ,hakuwa bonge wala modo alikuwa katikati ,si mnene si mwembamba ni watu wachache sana wanabahatika kuwa na maumbile kama haya ,ila kama ilivyokawaida kwa mwanadamu Mungu awezi kukujalia vitu vyote hata kama unavyo vingi ila kuna vingine huwezi kua navyo, ama kweli Mungu ni waajabu sana angempa binadamu mmoja vitu vyote nadhani duniani kungekua na majivuno ya hali ya juu ,Emmy alikuwa na tatizo kubwa sana ,tatizo lake alikuwa akijikojolea kitandani ,toka amezaliwa hadi sasa yupo kidato cha tatu lakini tatizo lake limekuwa ni sugu ,ilifika hata hatua mama yake mzazi aliwaza wenda mwanae kalogwa kwani hata kwa watoto wengi wakifikia umri wa miaka saba wanakuwa wameshaacha hiyo tabia ,wengine wakichelewa sana ni miaka kumi.
Mara nyingi sana Emmy alizuiliwa hata safari za kwenda mjini kwa ndugu zake hii ni kutokana na hali yake na tatizo lake ,,sifa ya kipekee aliyokuwa nayo emmy alikuwa ni mwongeaji ,emmy aliongea utadhania kafungiwa spika mdomoni ucheshi wake na sura yake ya kuvutia vilimfanya apendwe zaidi na marafiki zake waalimu na jamii pia
Baba mzazi na mama mzazi wa emmy walisugua kichwa kila kukicha waliwaza ,watakaa na binti yao hadi lini ,nyumbani ameharibu magodoro zaidi ya kumi ,magodoro yalikuwa yakitota mikojo kila kukicha ,emmy alikuwa na shida sana ,ilifikia wakati hata akijiegesha kitandani mchana anajikuta ameshajikojolea bila kujitambua ,wazazi wake walikuwa wakimwona akikimbilia bafuni tu ,wakiona hivyo wanajua amesahaharibu tayari ,kweli hali ya emmy ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa wazazi wake ,wazazi wake walimlindia siri mwanao kwa kipindi kirefu wakijipa moyo atakuwa sawa ila wapi
Siku moja majira jioni wakiwa nyumbani ,emmy alisikia sauti ya mtu akibisha hodi kwa haraka baba yake mzazi alisema ``Emmy ni kuwa husikii hodi hiyo au unajikalia tu hapa ‘’
Emmy alinyanyuka alipofika tu kwa haraka alikutana na binti anayeitwa sesilia ,sesilia ni ndugu kabisa na emmy ni mtoto wa mama mkubwa ,emmy alimkaribisha sesi ,,wote waliingia ndani ,baba na mama emmy walimkaribisha ,kwa sababu ilikuwa ni usiku sana sesilia alisema
``Mama mdogo leo mimi nitalala nimebeba na nguzo za shule kesho asubuhi nitaamkia hapa ‘’
``Sawa mwanangu usijali kabisa ‘’
Ilipofika muda wa kulala sesilia alipelekwa katika chumba cha wageni ,alipofikishwa tu alisema

``Mama mdogo mimi mwoga wewe acha tu Siwezi lala hapa mama naomba kulala na emmy ‘’
``mhhhh mwanangu haya kalale nae kama mtawezana ‘’
Sesilia aliingia moja kwa moja chumbani kwa emmy ,alipofika alimkuta emmy anapitiapitia daftari zake
``Shoga angu nimekuja tulale wote ‘’
``sawa dada karibu’’
Mama emmy alivyorudi chumbani mume wake alianza kumfokea
``Wewe mpumbavu sana unajua emmy anakojoa kama punda unategemea sesilia akijua nini kitatokea ‘’
``Mume wangu kanang’ania ‘’
``Wacha maneno yako haya sasa ngoja utaona kitakachotokea kesho’’
Ilipofika usiku wote walila ,kama kawaida wanafunzi huamka asubuhi sana hasahasa wanafunzi wa sekondari ,sesilia alipotaka kuamka aligusa unyevuunyevu wa kutosha ,alianza kujifikiria ,nimefanya nini mimi ,akili zake hazikumpelekea moja kwa moja kuwa ni emmy
Alipokaa vizuri alimtazama emmy ,maskini emmy nguo aliyovaa ilikuwa imetota mkojo mithili wa mtu aliyenyeshewa na mvua kubwa sana ,godoro lilikuwa limejaa maji ,
Sesilia aliangua kicheko kikubwa
``Mama yangu eeeeee hahahahaahahahahah emmy ,emmy ,emmy ,’’
Emmy alishikwa na aibu alijua lazima itakuwa anachekwa yeye
Sesilia alijitahidi kumwamsha mwenzake ila emmy alivunga sana  kama hajamsikia
Sesilia alikuwa na mdomo sana alitoka nje nakusema kwa nguvu
``Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni binti mkubwa ka wewe unakojoa haloooooo ‘’
Mama mdogo alipomwona na kumsikia sesilia alimwita na kumwambia
``Mwanangu usimcheke mwenzako siyo vizuri ni tatizo yuko nalo hili ni zoezi la kila siku ,baba yake mwaka hauishi lazima anunue godoro jipya kuwa mpole mwanangu sawa mbebee mdogo wako hii siri najua mnasoma nae darasa moja sawa ee’’
``Ok sawa mama’’
Sesilia aliitika kinafiki ila aliwaza saa ngapi anafika shule alihisi umbeya uta expire alioga haraka
Alivyoamka maskini alikutana na emmy ,kwa aibu kubwa emmy alipindisha macho chini kwa hofu kubwa sana alijua hapo seselia atamdharau sana
Baada ya dakika kumi na tano sesilia alibeba begin a kuwahi shule ,kabla hajafika shule alianza kutangaza kwa mashoga zake  ``EEEE shoga na ubuyu mrembo wa darasa hamna kitu ni kikojozi   aseee jana nimelala kwao yaan sema nimeoga tu hali siyo kabisa daaah ‘’
``Wacha shoga anakojoa huyooo ‘’
``hahahahahah Mungu wangu duniani kuna mambo ngoja nikawaambie na kina nancy na shoga ake kidawa maria Yule wanajikuta warembo hapa kumbe vikojozi’
Ndani ya dakika tano darasa zima lilijua na watu walimwamini sesilia kwani wanajua wazi ni ndugu yake
Ilipofika saa mbili emmy alionekana siku hiyo emy alichelewa kwani alikuwa akihofia sana kama sesilia kasema
Akiwa amesimama aliona kikundi cha marafiki zake  kikimfuata
``hahahahahahahh mrembo kikojozi hahahah eti unajikuta sister du haya sasa mama kitobo kinamwaga kama koki mbovu hahahahah makubwa kikojoziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kikojoziiiiiiiiiiiiii’’
Emmy alijua tu sesilia kashaharibu hali ,emmy kwa aibu alivyogeuka macho yake yaligongana ana kwa ana na sesilia ………….
Emmy atamfanya nini sesilia
Share plzzz nataka shares na komenti za kumwaga simulizi hii nataka iishe mapema kabisaa ina uhondo wakila namna utajifunza vingi sana wewe mzazi ,mtoto ,binti ,simulizi haibagui kila mtu lazima ajifunze
Wale mnaopenda simulizi zangu karibu nikuunge kundi langu whatsapp upate simulizi zangu kwa wakati ,gharama ya kuungwa ni sh 1000 tu lipa kwa 0742873299 Martha shao ukimaliza nitafute whatsapp kwa 0742873299 au 0713111547 nikuunge ,hatuungi kundi bure nieleweke ,karibu sana

GUSA HAPA KUUNGWA WHATSAPP

Post a Comment

1 Comments