MUME WA MTU SUMU (1)

MUME WA MTU SUMU (part one)
NA J,SHAO
0713111547 WHATSAPP
``Rebekaaaa rebekaa mke wangu rebekaaa njoo mama nikwambie japo maneno ya mwisho maana kifo kishabisha hodi nimebakiza dakika chache za kuishi  mke wangu’’
``khaaaaa na wewe  mwanume nasema kama unakufa kufa usinipigie kelele hapa khaaaa’’
``mke wangu rebeka njoo nikuachie maneno ya mwisho kipenzi njoo tafadhali ‘’
``siwezi kuja nipo nachat nashoga angu levina’’
Baba caren alipoona anakaribia kukata roho aliita kwa nguvu ``caren mwanangu njoo ‘’
Caren alikua ndio anatoka shule darasa la pili kwa mbali alisikia sauti ya baba yake mzazi ,caren alimpenda sana baba yake na kwa jinsi alivyokuwa mgonjwa mara nyingi alikaa pembezoni mwa kitanda chake huku akimpatia maji na chakula ni kazi ngumu sana ambazo alipaswa afanye   mama yake ila mama yake ajulikanae kama rebeka alikua na roho ya kikatili  mno ,roho yake  hata  mnyama ana nafuu
Caren alikimbia haraka kuelekea   Alipo baba yake ,caren alipofika kitandani alichuchumaa nakumshika baba yake mkono huku kipiga kelele kubwa ``baba usife usife baba angu nakupenda baba ,baba sinilikwambia nitasoma niwe daktari nije nikutibu baba angu nakupenda sana baba usife baba’’
Kwa kigugumizi baba caren alisema ``mwanangu nakupenda sana ila na lakukwambia najua wewe ni mdogo sana siyo vyema kukwambia ila mwanangu sikia`` kuwa makini na ma-ma mama ako si—‘’ alipokuwa akitaka kumalizia maneno yale alijikuta akishindwa ila alijikaza na kusema
``mama yako si mtu mzuri jihadhari nae msikilize mama mkubwa na shangazi utafika mbali’’
Alipomaliza kusema hivyo baba caren alitupa mikono na kufa hapo hapo
Caren kwa uchungu alilia kwa sauti kubwa ``baba usifeeeeee baba angu eeee baba jamaniii baba’’
Ila ndio ilikua ndio hivyo baba caren alifia mikononi mwa mwanae kipenzi ,caren kwa haraka alichomoka hadi alipo mama yake ,alimkuta mama yake akiwa amenyanyua miguu juu masikioni kavalia headphone (spika za masikioni) huku ameshikilia simu mkononi akiperuzi
Caren aliita kwa haraka ``mama njoo mwangalie baba amekufa njoo mama jamani’’
Mama caren aitwae rebeka alisunya ``nyooooo afe vizuri kabisa ana nini huyo kazi kulalala tu na kutumalizia oksijeni humu ndani alafu njoo hapa wewe useme baba ako kakwambia nini bila shaka kuna kitu kasema kabla hajafa ‘’
Caren alitumia akili alijua akisema aliyoambiwa itakua ni tatizo mama yake aliendelea kukazia
``njoo hapa wewe kunguni baba ako kakwambiaje ‘’ mama caren alivuta sikio la caren na kumlazimisha aseme
Caren aliendelea kushikilia msimamo hakusema kitu
Mama caren kwa hasira  alimzaba kibao cha nguvu caren ``paaaaaah wewe nyang’au unajitia mjuaji sasa tutaona utakaa na nani au utaenda kuishi na baba yako mochwari ‘’
Caren hapo ndio alianza kutambua maneno ya baba yake kuwa mama yake siyo mzuri
Caren aliona cha msingi ni kukimbia ,caren alikimbia na kufika njee alipiga kelele
``msaada jamani baba amekufa ,baba amekufa ,baba amekufaa’’
Watu waliokuwa wakipita na majirani waliposikia walikuja haraka nakuingia ndani
Rebeka alivyo mnafiki alichukua kanga na kujitanda huku akilia kwa unafiki
``jamaniii mume wangu kipenzi uwiiiiiiii  umeniacha mimi na mwanangu caren tutaishije jamani uwiiiii kwanini Mungu hauna huruma ila yote ni mpango wako ‘’
Watu walimfuata na kumbembeleza ,caren hakuamini alipoona mama yake anaigiza namna ile
Watu walimfuata na kumtuliza kwani alikua akijitupa tupa na kulia bila kutoa machozi ,kwa kweli duniani kuna vioja
Baada ya siku mbili harakati za mazishi zilikwisha baba caren aliwekwa kwenye kaburi nyumba yake ya milele ,ilikua ni huzuni kwa  caren ,caren alikua akimpenda sana baba yake kuliko chochote toka alipozaliwa baba yake alikua nae karibu sana
BAADA YA SIKU 3
Siku tatu tu baada ya msiba katika nyumba ya rebeka mama yake na caren lilionekana gari aina ya rava4 likiwa limefunga breki hapo ,ndani ya gari lilishuka jibaba lenye kitambi kikubwa na kupitiliza ndani
Caren akiwa sebuleni mama yake alimwambia ``weee caren  nenda chumbani kapumzike niongee na anko ‘’ caren aliondoka
Jibaba lile lilimkamata mama rebeka na kumshushia makiss kama mvua alipomaliza alimwambia
``hongeraaa san asana si nilikwambia ile sumu ni hatari sana inaua taratibu unaona toka nimekupa haijapita hadi wiki mumeo kafa sasa ni wakati wetu wa kula maisha haahah mwanamke wewe mbichi mbichi rebeka wangu ni mwendo wa kula vinono tu kwanza ndio una mtoto mmoja hujatumika kivile natamani hata nikufanye mke wa pili’’
Rebeka kusikia vile alirembusha macho na kumkiss boss Yule walichezeana sana ,,,rebeka alimshika mkono tajiri Yule na kumpeleka katika chumba chake ambacho walikua wakilala na mumewe ,,
Rebeka alilala na tajiri walifanya kufuru walifanya yote waliyoweza kufanya ,tajiri Yule alijikuta akisema
``patamu hapaaaa yaan rebeka utanifanya nimwache mke wangu kabisaaa mama ulivyo fundi’’
Ilipofika saa tatu za usiku tajiri Yule alichukua gari lake na kumwaga rebeka
Rebeka alirudi ndani na kuandaa mayai ya kukaanga kisha alimpa mwanae na juisi ale akimaliza alale ,,
Ndani ya dakika tano gari aina ya spacio lilifunga breki nje ya nyumba ya mama rebeka
Mama rebeka ndio alikua ametoka kuoga kutokana na shughuli aliyotoka kufanya muda siyo mrefu
Aliposikia sauti ya gari lililofunga breki kwa nje kwa haraka alikimbia na kwenda kumpokea alijua atakuwa ni benny
Benny alikua ni mfanyabiashara mkubwa sana aliyekua akichukua mizigo kutoka dubai kuleta Tanzania alikua na fedha kama utitiri yeye na mkewe walipendana  ila kwa siri benny alikua akichepuka mkewe hakuwahi tambua hili
Benny alipokwisha paki gari nje ya nyumba ya rebeka aliingia ndani ,aliingia kwa ujasiri kwani alijua mume wa rebeka ameshakufa ,,benny alipoingia ndani rebeka alimpa makiss mazito huku akiongea maneno ya mahaba
``jamaniiii benny wangu darling sweetheart nimekumiss toka saa kumi na mbili nakusubiri wewe unakuja saa tatu jamani’’
``hahah samahani love ‘’
Walichukuana hadi chumbani ,walijitupa kitandani na kufanya yao
Upande wa pili tajiri Yule aliyeondoka kwa rebeka muda siyo mrefu akiwa njiani alikumbuka raha alizopewa na rebeka alisema
``mama angu eee huyu rebeka anajua siyo siri sasa hapa mimi ni kujilia tu ,,hakika watoto wakitanga wanajua mapenzi hizi raha sijawahi pata eti popote’’
Kwa haraka tajiri alipiga mkono mfukoni kuchukua simu yake mfukoni ,alipopiga mkono mfuko alishangaa simu haipo alijua lazima itakuwa tu ameisahau kwa rebeka kwani walipokuwa wakifanya mapenzi simu ilikua pembeni ya kitanda
Tajiri alikata kona na kurudi kwa rebeka
Rebeka aliendelea kufanya uchafu na benny ,benny mfanyabiashara alikua akipiga kelele tu za furaha kwani mambo aliyokuwa akiyafanya benny si ya nchi hii
Tajiri alipokaribia kwa rebeka alishangaa kuona gari likiwa limepaki nje pale alisema
``macho yangu haya ama vipi ni nani huyu kapaki hapa ,,,mhhh rebeka hawezi nisaliti mimi nimempa hadi sumu amuue bwana wake tuishi wote atanifanyiaje mimi uhuni khaaaa haiwezi tokea ‘’
Boss alishuka ndani ya gari na kusogea hadi karibu na dirisha akiwa nje alisikia makelele kwa ndani
``benny nakupenda baba ni wewe tu hamna mwingine niamini’’
Zilikua ni kelele za rebeka akifurahia mchezo wao mchafu aliokuwa akifanya na mfanya biashara mkubwa benny
Tajiri Yule hakuamini masikio yake kwa hasira alirudi ndani ya gari na kuchomoa bastola

Je nini kitaendelea …………………………………………….fuatilia page
Rebeka atapona benny je
Jipatie simulizi hii nzima SASA WASILIANA NAMI 0742873299 SMS

Post a Comment

0 Comments