SIKIA KILIO CHANGU MAMA


SIKIA KILIO CHANGU  (1)
MTUNZI JOSHUA SHAO
0713111547 WHATSAPP
Sauti ya kichanga iliendelea kusambaa sehemu zote katika eneo lile la kutupa  takataka ,huwezi amini watu waliokuwa pale walikuwa wala hawakujigusa  wala kuona kama ni kero walikuwa wakisema
``Yaan hapa ukisema ukote vichanga utaokota vingapi kila kukicha lazima vitupwe ,wasichana wa mtaa huu wameoza sijui hata tutawafanyaje wameshajitoa ufahamu kabisa kabisa ‘’
Mama mmoja alipita karibu na jalala lile  kelele za kichanga kile zilipenya moja kwa moja kwenye masikio yake , mama Yule uvumilivu ulimshinda alisoge moja kwa moja kilipo kichanga kile kutazama kelele zile zinasababishwa na nini
Maskini mtoto alikuwa amesokotwa ndani ya kanga na kutupwa ndani ya jalala la takataka kisha alisukumiziwa  rundo la uchafu .hakika nilikuwa siamini maneno ya watu walipokuwa wakisema
``Binadamu aliyepoteza utu ni sawa na mnyama ‘’
Hakika huu ni unyama uliopitiliza ,vijana wanasema ``Unyama unayamani ‘’ ama kweli  huu ni zaidi ya unyama
Piala ni msichana aliyezaliwa katika familia ya kitajiri sana ,baba na mama yake walikuwa na uwezo mkubwa kupita kiasi ,nyumbani kwao walikuwa wamewaajri wafanyakazi wa kutosha ,kulikuwa na zaidi ya vijana saba wakufanya shughuli mbalimbali Piala pamoja na ndugu yake waliishi kama mabosi
Piala alikuwa na jeuri sana huwezi amini akiwa na umri wa miaka kumi na tisa mwanamke mzima mwenye manyonyo alikuwa akitawaza ili tu kuwakomoa na kuwatesa wafanyakazi wa nyumbani
Siku moja Piala  akiwa chooni mchana aliita kwa nguvu
``We thedy njoo upesi ‘’
Tedy mfanyakazi wa nyumbani alitulia kimya aliona ni ngumu kwenda chooni  wakati bado mtu anajisaidia
Piala alianza kutukana kwa nguvu
``wewe mavi wewe umegoma kuja siyo sasa leo lazima uondoke uende kwenu kijijini naona kukaa hapa kumekushinda pumbavu na nusu ‘’
Thedy kusikia hivyo alikimbia moja kwa moja hadi chooni
Alipoingia ndani alimkuta piala akiwa anafanya yake taratibu
Thedy aliziba macho kwa aibu huku akisema
``Piala kitu gani umeniitia ‘’
Piala bila haya wala aibu alisimama akiwa uchi na kuegemea ukuta kisha akamwambia binti wa kazi ``Haya nitawaze upesi ‘’
Thedy alijibu ```PIALA haiwezekani mambo gani haya unaniitia acha kunifanyia hivyo binadamu mwenzio ‘’
                ``Unasemaje ???’’ aliiuliza kwa hasira
Thedy aliona hali itakuwa mbaya kwa haraka alichukua nailoni zilizookuwa pembeni na kuzivaa
Piala alimtemea mate usoni na kumwambia `` Mpuzi wewe unanivalia nailoni mimi maiti nakwambia toa upesi na nitawaze haraka ‘’
Maskini watoto wa ma bosi shida tupu huwezi amini  thedy alianza kumtawaza piala kwa mikono yake alishika mavi ya mwanamke mzima`` ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni ‘’ hakika hiii ilikuwa ni hatari sana uhuni usoelezeka.
Thedy alipomaliza alitoka nje huku akiimba kwa uchungu sana kujifariji alikuwa akiimba wimbo
``Ipo siku yangu tu nami nibaniba nibarikiwe ‘’
Piala alisunya na kumwambia ``Maskini ni maskini tu na miaka yako ilivyoenda lini utabarikiwa wewe nakwambia utakuwa house girl maisha yako yote mbwa wewe’’
Hakika piala alikuwa na kiburi  na majivuno ya hali ya juu ,yaani ulikuwa ukimtazama unaweza sema kwanini wewe sio Mungu umrushie nyiwe au umpige na radi umsambaratishe mbali kabisa
Ila ndio hivyo piala aliendelea kutesa kwa zamu alikuwa akiwatumikisha wafanyakazi wa baba yake jinsi apendavyo ,aliishi kama bosi kitanda alitandikiwa nguo alifuliwa hiyo tuu haitoshi aliwatesa sana wafanyakazi wa baba yake
Mbali na upuzi huo piala alikuwa ni mwanamke mshenzi sana ,alikuwa anafanya ufuska wa kila aina ila alikuwa akificha sana kwani baba yake alikuwa anatamani sana kumwona mwanae akipiga hatua kimasomo na kimaisha mzee Petro alijitahidi sana kumlea piala alimpa kila kitu alimletea waalimu wa kutosha nyumbani kwa ajili ya kumfundisha ili siku moja aweze kufika mbali kimaisha
Piala alikuwa ni muhuni sana huwezi amini piala yeye mwenyewe ndiye alikuwa akiwatongoza wanaume ,alikuwa akisha mpenda mkaka lazima ampate atafanya juu chini kuhakikisha amempata
Ilikuwa mwezi wa kwanza piala baada ya kutoka shule akiwa amepumzika sebuleni alimwona baba yake akiongozana na kijana mmoja mwenye mwili uliojijenga kiume ,kijana huyo alikuwa na misuli na kifua cha mazoezi ,piala alipomwona kijana Yule moyo ulipasuka paah alijisemea
``Eee Mungu awe ni mfanyakazi tu ‘’ na kweli kijana  Yule alipewa chumba ,alifanywa mfanyakazi wa pale nyumbani
Usiku huo huo piala alimtokea kijana Yule kisha alianza kumwonyesha dalili za kumtaka ,huwezi amini kijana Yule baada ya kuonyeshwa laki moja na piala alikuwa mpole kama maziwa ya mtindi ‘’
Piala alirusha roho na kaka wa watu
Baada ya miezi mitatu piala alianza kujihisi tofauti mara kichefuchefu mara hasira mara usingizi
Piala alijua hii ni mimba kwa haraka aliwenda duka kubwa la dawa na kumweleza muuzaji kuwa ana mimba ,piala alimpatia takribani shilingi laki mbili
Muuzaji Yule alimpatia dawa ambayo akimeza tu dakika 40 mimba inatoka
Piala alimeza hapohapo kisha aliondoka moja kwa moja kwa kukimbia
Huwezi amini piala alipofika nyumbani nje ya mlango wake damu zilianza kuvuja kwa haraka alikimbia ndani .mimba ile ilitoka ,piala alikusanya mauchafu yote ya mimba iliyoharibiwa na kutoka nje kwa siri sana kwenda kutupa
Thedy binti wa kazi alishtuka alijua kabisa piala amefanya uasi alianza kuongozana nae nyuma piala alielekea moja kwa moja hadi  sehemu ya kutupa matakataka kisha akatupa  mfuko uliokuwa na uchafu wa mimba aliyoitoa ,piala aliangalia kushoto na kulia kujiridhisha kuwa hakuna ambaye amemwona
Aliporudisha mguu nyuma na kuondoka thedy aliyekuwa amejificha kwa uzio alichomoka na kukimbilia mfuko ule kisha kwa kejeli alicheka kwa nguvu
``hahahahahahahaha leo umepatikana ‘’
Piala aligeuza kichwa nyuma ,alihisi kuchanganyikiwa miguu ilishikwa na ganzi alitetemeka hakutaka kabisa mtu ajue alichokifanya ,wala hakutaka hata baba yake ajue kuwa alikuwa na mimba
Piala alimtazama thedy kwa kumkazia macho
Je nini kitaendeleaaa…………………SHARE TAFADHALI
Hii ni stori yenye ladha ya aina yake ina mikasa ya kushangaza sana na kusisimua  IPO TAYARI YOTEEEE

Unasubiri nini lipa  1000  tu kusoma yote lipa kwa namba 074287399 mpesa ukimaliza nitumie meseji kuwa tayari nikutumie simulizi whatsapp au facebook ila whatsapp napatikana kwa namba 0713111547
NUNUA SIMULIZI ENDELEZA SIMULIZI ZA JOSHUA









Post a Comment

0 Comments